• HABARI MPYA

    Wednesday, April 03, 2019

    WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUTANGAZA UTALII KUPITIA MICHUANO YA AFCON U17

    Na Anitha Jonas – WHUSM, DODOMA
    SERIKALI ya dhamiria kutumia jukwaa wa Mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika hivi karibuni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kunufaika na wageni mbalimbali watakao kuja kushiriki michuano hiyo ya Kimataifa.
    Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa lengo la kuhakiki mikakati itakayotumika kutangaza vivutio hivyo ambavyo ni tunu ya Taifa.
    “Sisi Wizara ya Maliasili na Utalii tutahakikisha tunatumia jukwaa hili la michezo kuongeza idadi ya watalii katika vivutio vya utalii nchini na tumejipanga vizuri kwa matangazo mbalimbali ambayo yanamvuto wa ushawishi kwa watalii hawa wamichezo kuvutiwa kufika katika maeneo hayo tunafukwe nzuri,Mbuga za wanyama,majengo ya kale yenye hishoria mbalimbali,maporomoko ya maji na Mlima Kilimanjaro,”alisema Prof. Mkenda.
    Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Prof. Mkenda alisisitiza kuwa ujio wa mashindano hayo ya AFCON U17 nchini ni jambo lenye manufaa makubwa kwa taifa kwani kwa kujipanga vizuri huu ndiyo wakati wa kunufaika kwa watanzania wote kupitia wageni hao, wajasiriamali mbalimbali watanufaika kwa namna moja kwani wageni hao watahitaji huduma mbalimbali kwa kipindi chote watakapo kuwa hapa nchini hivyo ni vyema watanzania watumie fursa hii.
    Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Susan Mlawi alitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo tunashukuru sana kwani fedha hizo zitasaidia kukamilisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika kipindi cha mashindano.
     “Wizara yangu kama mlezi wa Sekta ya Michezo Nchi  mpaka sasa tumesha kamilisha mambo muhimu yote tuliyoagizwa CAF na vimebaki vitu vidogo sana ambavyo vitakamilika ndani ya muda mfupi hivyo naweza kusema tupo tayari kwa mashindano,”alisema Mlawi.
    Pamoja na hayo nae Mlawi alieleza  kuwa mashindano hayo yanataanza Aprili 14, Mwaka huu na Mechi ya ufunguzi inatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kujipanga kwa ugeni huu na watanzania nivyema kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa taifa letu kuandaa mashindano haya ya Kimataifa.
    Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao alieleza kuwa katika mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino atakuja hivyo ujio wake katika mashindano hayo utakuwa ni fursa ya kutangaza nchi yetu, vilevile uongozi wote washirikisho la mpira wa Miguu Afrika  (CAF) nao utahamia Tanzania katika kipindi chote cha mashindano.
    “Katika mashindano hayo ndipo wadau wa soka duniani wanakuja kusaka vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuwaunga katika timu zao kubwa za kimataifa mfano mchezaji kama Neymar ni mmoja ya wachezaji waliyoibuliwa katika mashindano ya mpira kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 hivyo wapo wadau mbalimbali duniani watakuja kwa ajili ya hilo,”alisema Kidao.
    Wito kwa watanzania ni kuwa tayari kwa ujio huu wa kimataifa na kujipanga vyema kunufaika na wageni hawa kwa kuhakikisha wanakuwa watulivu na wakarimu kwa ajili ya kuiletea nchini mafanikio katika uchumi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUTANGAZA UTALII KUPITIA MICHUANO YA AFCON U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top