• HABARI MPYA

  Friday, August 17, 2018

  TYSON FURY NA DEONTAY WILDER WATAKA KUZIPIGA 'KAVU KAVU'

  MABONDIA Tyson Fury na Deontay Wilder jana walitaka kupigana wakati zoezi la kupima uzito kwenye hoteli.
  Wilder alisafiri kwenda Belfast kutoka Marekani kumuona Fury akipima uzito na kuonyesha amekuwa mwepesi baada ya muda mrefu tangu alipotwaa ubingwa wa dunia kwa kumdunda Wladimir Klitschko.
  Fury anatarajiwa kupigana na Mmarekani huyo anayesifika kwa ngumi zake nzito, iwapo atafanikiwa kumshinda Mtaliano Francesco Pianeta Uwanja wa soka wa Windsor Park, Jumamosi.
  Wilder ndiye aliyeanza kumbeza Tyson ambaye alikasirika na kutaka kuzichapa 'kavu kavu' na Mmarekani huyo. Baba wa Fury, John akaingilia kati kwa kujibizana na Wilder.

  Tyson Fury na Deontay Wilder jana walitaka kupigana wakati zoezi la kupima uzito kwenye hoteli  

  Wilder akamuambia baba yake Tyson Fury; "NItamfufua babu yangu kaburini kwake aje akupige wewe mzee.’
  Wilder pia akamkandia Anthony Joshua kwa kusema: "Tyson atashinda Jumamosi usiku na kisha nitampiga mimi tukikutana. Joshua ni habari za zamani. Mtoto mpya mjini ni Fury na letu ni pambano kubwa,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY NA DEONTAY WILDER WATAKA KUZIPIGA 'KAVU KAVU' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top