• HABARI MPYA

  Saturday, August 18, 2018

  REAL WAISHITAKI INTER MILAN FIFA KUTAKA KUMSAJILI MODRIC

  KLABU ya Real Madrid imeishitaki Inter Milan Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa kutaka kumsajili kiungo wao, Luka Modric kinyume cha utaratibu. 
  Msemaji wa FIFA amethibitisha kwamba bodi hiyo ya soka duniani imepokea malalamiko kutoka klabu ya Hispania dhidi ya vigogo wa Serie A kutaka kumsajili mwanasoka huyo wa kimataifa wa Croatia, Modric.
  Kutokana na dirisha la usajili la Italia kufungwa jana, Inter imefeli kumsajili mchezaji huyo kwa kumng'oa Modric Bernabeu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alitokea benchi kipindi cha pili atika mechi ya UEFA Super Cup dhidi ya Atletico Madrid Jumatano, wakifungwa na Atletico Madrid 4-2 baada ya dakika 120.

  Luka Modric anazigombanisha Real Madrid na Inter Milan na kesi imefika FIFA

  Hicho kilikuwa kipigo cha kwanza cha Real tangu imuuze nyota wake, Cristiano Ronaldo klabu ya Juventus kwa Pauni Milioni 100 na tangu kocha Zinedine Zidane ampishe aliyekuwa kocha wa Hispania, Julen Lopetegui.
  Modric alijiunga na Real kutoka Tottenham mwaka 2012 na ametwaa taji moja la La Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL WAISHITAKI INTER MILAN FIFA KUTAKA KUMSAJILI MODRIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top