• HABARI MPYA

  Saturday, August 11, 2018

  SIMBA SC YABANWA NA NAMUNGO FC RUANGWA, SARE 0-0 UWANJA WA MAJALIWA

  Na Mwandishi Wetu, LINDI
  KIKOSI cha Simba SC kimelazimishwa sare ya bila kufungana na Namungo FC ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
  Hiyo inakuwa sare ya pili mfululizo kwa mabingwa hao wa Tanzania, baada ya Jumatano pia kutoka sare ya 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo mwingine wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mchezo wa leo ulikuwa maalum wa kuzindua Uwanja wa Majaliwa unaotokana na jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Kassim Majaliwa. 
   
  Kwa Simba SC, mchezo huo ulikuwa sehemu ya maandakizi ya mchezo wake wa Ngao ya Jamii Agosti 18 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YABANWA NA NAMUNGO FC RUANGWA, SARE 0-0 UWANJA WA MAJALIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top