• HABARI MPYA

  Saturday, August 11, 2018

  KMC YAITUPA NJE KWA MATUTA MTIBWA SUGAR KOMBE LA REHA TEMEKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC leo imeibuka na ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Kombe la Reha Day Uwanja wa Bandari, Tandika mjini Dar es Salaam.
  Hiyo ilikuwa ni baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 90 katika mchezo huo mzuri uliohudhuriwa na mashabiki wachache jioni ya leo.
  Mtibwa Sugar inayofundishwa wachezaji wake wa zamani, kocha Zubery Katwila anayesaidiwa na Patrick Mwangata chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Mayanga leo ilishindwa kufurukuta mbele ya KMC.

  KMC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu na kukisuka upya kikosi chake chini ya aliyekuwa kocha wa Mbao FC ya Mwanza kwa misimu miwili iliyopita, baada ya kuikosa Mtibwa katika dakika 90 ikaenda kuimaliza kwenye matuta.
  Na kwa matokeo hayo, KMC itakwenda kukutana na Transit Camp iliyoitoa Reha FC kwa penalti 3-0 baada ya sare ya 0-0 pia katika mchezo uliotangulia leo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAITUPA NJE KWA MATUTA MTIBWA SUGAR KOMBE LA REHA TEMEKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top