• HABARI MPYA

    Thursday, August 16, 2018

    NI ATLETICO MADIRD WASHINDI SUPER CUP YA UEFA…WAIPIGA REA 4-2

    TIMU ya Atletico Madrid imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kuwania taji la Super Cup ya Ulaya usiku huu Uwanja wa A. Le Coq Arena mjini Tallinn, Estonia.
    Shujaa wa Atletico Madrid leo amekuwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Diego Costa aliyeipasua ngome ya Real Madrid mara mbili. 
    Costa alifunga bao la kwanza mapema tu dakika ya kwanza akimalizia pasi ya Diego Godin, lakini mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema akaisawazishia Real dakika ya 27 akimalizia pasi ya Gareth Bale.

    Atletico Madrid wakifurahia na taji lao la UEFA Sper Cup baada a ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Real Madrid 

    Nahodha, Sergio Ramos akaifungia bao la pili Real Madrid kwa penalti dakika ya 63, baada ya Juanfran kuushika mpira kwenye boksi.
    Coasta akarejesha matumaini kwa Atletico baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 79 akimalizia pasi ya Muargentina, Angel Martin Correa na dakika 90 zikalazimika timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.
    Saul Niguez Esclapez akaifungia Atletico Madrid bao la tatu dakika ya 98 akimalizia pasi ya kiungo Mghana, Thomas Teye Partey na Jorge Resurreccion Merodio, maarufu kama Koke akaifungia bao la nne timu hiyo dakika ya 104 akimalizia pasi ya Víctor Machin Perez au Vitolo kwa jina maarufu zaidi.
    Real Madrid leo walikuwa wanacheza mechi ya kwanza ya ushindani tangu waachane na kocha wao, Mfaransa Zinadine Zidane na nyota wao, Cristiano Ronaldo waliyemuuza Juvuntus Pauni Milioni 100 mwezi uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI ATLETICO MADIRD WASHINDI SUPER CUP YA UEFA…WAIPIGA REA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top