• HABARI MPYA

  Friday, August 17, 2018

  MTOTO WA RONALDINHO AKATAA UTAMBULISHO WA BABA YAKE

  MTOTO wa Ronaldinho alijaribu kuficha utambulisho wake halisi wakati wa majaribio kwenye klabu ya Cruzerio ya Brazil.
  Mtoto huyo wa gwiji wa soka Brazil, Joao Mendes, akiwa ana umri wa miaka 13 tu tayari ameanza kufanya vyema katika soka ya vijana.
  Alifanya majaribio Paris Saint-Germain, moja ya klabu nyingi alizochezea baba yake, kwenye Uwanja wao wa mazoezi mji mkuu wa Brazil, Brasilia kabla ya kwenda Cruzeiro, ambao timu yao ya wakubwa inashiriki Ligi Kuu.
  Lakini, kwa mujibu wa gazeti la Globoesporte la Brazil, Mendes alitaka kupanda zaidi kupitia mfumo wa soka ya vijana ya klabu hiyo, kuliko kwenda kwenye klabu kubwa inayomtaka kwa sababu ya jina la baba yake.

  Mtoto wa Ronaldinho mwenye umri wa miaka 13, Joao Mendes (kulia) anaibukia vizuri kisoka; Hapa akiwa na mama yake, Janaina Nattielle, na Jorge Washington anayefanya kazi na klabu ya Cruzeiro ya Brazil

  Mendes anazaliwa na mama, Janaina Nattielle Mendes, dansa wa zamani aliyeoolewa na gwiji wa Barcelona mwaka 2004 ingawa ndoa yao ilivunjika miaka miwili baadaye, 2007. Na mama yake ndiye anamle mtoto huyo na ndiye mwenye maamuzi yote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTOTO WA RONALDINHO AKATAA UTAMBULISHO WA BABA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top