• HABARI MPYA

  Wednesday, August 15, 2018

  HIMID MAO ‘MOTO CHINI’ LIGI KUU YA MISRI, LAKINI PETROJET YATOA SARE 2-2

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami, timu yake, Petrojet FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Al Masry Jumanne katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.
  Himid Mao aliye katika msimu wake wa kwanza Petrojet alicheza vizuri kwenye mechi hiyo nzuri, lakini akashuhudia timu yake ikilazimishwa sare ya tatu mfululizo kwenye Ligi katika mechi nne walizocheza, moja wakishinda.
  Islam Issa alianza kuwafungia Al Masry dakika ya 23, kabla ya mshambuliaji Muivory Coast, Mohamed Sanogo Vieira kuisawazishia Petrojet dakika ya 43. 
  Himid Mao (wa pili kulia) na timu yake, Petrojet FC mjini Alexandria, Misri. 

  Ahmed Gomaa akaifungia tena Al Masry bao la kuongoza dakika ya 52, lakini kwa mara nyingine Vieira akaisawazishia Petrojet dakika ya 69.
  Kwa matoeko hayo, Petrojet inabaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi 16, kwa pointi zao sita za mechi nne, wakati Al Masry inabaki nafasi ya tano kwa pointi zake nne za mechi tatu. Smouha inangoza Ligi Kuu ya Misri kwa pointi zake saba sawa na El Entag El Harby baada ya wote kucheza mechi tatu.
  ndishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami, timu yake, Petrojet FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Al Masry Jumanne katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.
  Himid Mao aliye katika msimu wake wa kwanza Petrojet alicheza vizuri kwenye mechi hiyo nzuri, lakini akashuhudia timu yake ikilazimishwa sare ya tatu mfululizo kwenye Ligi katika mechi nne walizocheza, moja wakishinda.
  Islam Issa alianza kuwafungia Al Masry dakika ya 23, kabla ya mshambuliaji Muivory Coast, Mohamed Sanogo Vieira kuisawazishia Petrojet dakika ya 43.  
  Ahmed Gomaa akaifungia tena Al Masry bao la kuongoza dakika ya 52, lakini kwa mara nyingine Vieira akaisawazishia Petrojet dakika ya 69.
  Kwa matoeko hayo, Petrojet inabaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi 16, kwa pointi zao sita za mechi nne, wakati Al Masry inabaki nafasi ya tano kwa pointi zake nne za mechi tatu. Smouha inangoza Ligi Kuu ya Misri kwa pointi zake saba sawa na El Entag El Harby baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO ‘MOTO CHINI’ LIGI KUU YA MISRI, LAKINI PETROJET YATOA SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top