• HABARI MPYA

  Tuesday, August 14, 2018

  TWIGA STARS KUSHIRIKI MICHEZO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, MICHUANO KUANZA ALHAMISI BURUNDI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi amewataka wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika Bujumbura nchini Burundi kwenda kufany vyema.
  Akizungumza katika hafla maalum ya kuwaaga na kuwakabidhi bendera, Susan amesema kwamba ana imani kubwa maandalizi yamekuwa mazuri na sasa ni kwenda kupigania heshima ya nchi katika mashindano hayo yanayoanza kutimua vumbi Alhamisi mjini Bujumbura.
  Tanzania itawakilishwa na vikosi vinne katika michezo ya Riadha, soka ya wanawake, Karate na Netiboli ambao wote wanamichezo wake walikuwepo kwenye hafla ya kukabidhiwa bendera.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi (kulia) akiwakabidhi bendera wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika Bujumbura 

  Upande wa Riadha kuna wakimbiaji wanane ambao ni Ally Khamis Gulam mita 100 na 200, Michael Zachariah Gwandu kuruka vihunzi, Fabiano Nelson Sulle, Marco Joseph, Natalia Elisante Sulle, Anjelina Joseph Yumba wote mbio ndefu, Rose Seif mita 200 na 400, Neema Paulo Gadiye mita 800 na 1500 na viongzi wao wawili, Rehema Abdallah Killo na kocha Mafunda Khamis Juma.
  Kwenye mpira wa miguu na kikosi cha timu ya taifa ya wanawake, maarufu kama Twiga Stars kinachoundwa na Fatuma Omar, Najiath Abbas, Gerwa  Yonah, Wema  Richard, Fatuma  Bushiri, Stumai  Abdalla, Maimuna  Khamis, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Happy Hezron, Asha Hamza na Amina Ally.
  Wengine ni Donisia  Daniel, Mwanahamis Omari, Asha  Rashid ‘Mwalala’, Fatuma Mustapha, Enekia  Kasongo, Irene  Kisisa, Kocha Mkuu Hababou Ali Omary, Msaidizi wake Edna Lema, Daktari Richard Yomba, Meneja Zena Chande na Esther Chaburuma.
  Katika Karate wapo wanamichezo sita ambao ni Mikidadi Kilindo, Abdul Mussa, Mohamedi King’ara, Ally Makuka na Swedi Fundukira pamoja na kocha wao, Yahya Mgeni.
  Katika Netiboli wapo Fatma H. Machenga, Zuhura Twalib, Matalena Mhagama, Dawa Haji, Agnes Nyalusi, Mary Kajigiri, Sophia Komba, Lilian Sylidion, Restuta Boniface, Ashura Ramadhan, Monica Aloyce, Bhoke Juma Kocha Mwajuma Kissengo na Kiongozi wao, Judith Ilunda.
  Msafara utaongozwa na Addo Antony Komba, Meneja Benson John Chacha, Daktari Christine Cosmas Luambano na Kiongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Khamis Ali Mzee.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS KUSHIRIKI MICHEZO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, MICHUANO KUANZA ALHAMISI BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top