• HABARI MPYA

  Wednesday, August 15, 2018

  DE BRUYNE AIBUA HOFU KUBWA MAN CITY BAADA YA KUUMIA LEO

  Mshambuliaji Mbelgiji, Kevin De Bruyne ameumia mazoezini Manchester City 

  NANI KUZIBA PENGO LA KEVIN DE BRUYNE  

  Nani ataziba pengo la De Bruyne kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City?
  Bernando Silva, Riyad Mahrez na Ilkay Gundogan
  KLABU ya Manchester City imepata pigo baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Kevin De Bruyne kuumia mazoezini leo.
  Hofu kubwa imetanda kwamba De Bruyne amepata maumivu makubwa kwenye mguu wake wa kulia na City wanahofia wanaweza kumkosa tegemeo lao huyo kwa miezi mitatu.
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 27 atakwenda kufanyiwa vipimo zaidi kujua ukubwa wa maumivu yake, lakini habari hizi ni pigo kwa kocha Pep Guardiola.
  De Bruyne alipigwa picha akiwa gym wakati wa mazoezi ya asubuhi kabla ya baadaye kuumia kwenye mazoezi ya mchana uwanjani.
  Man City imetoa taarifa rasmi ikithibitisha De Bruyne atakwenda kufanyiwa vipimo zaidi.
  Maumivu aliyoyapata ni sawa na ya mwaka 2016 wakati De Bruyne alipolazimika kuwa nje kwa wiki tisa baada ya kuumia wakati akikabiliana na Ramiro Funes Mori wa Everton.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BRUYNE AIBUA HOFU KUBWA MAN CITY BAADA YA KUUMIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top