• HABARI MPYA

  Monday, August 13, 2018

  BATENGA PEKEE AREJESHWA KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SC, MWENYEKITI MPYA LYAMWIKE

  Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWANACHAMA  maarufu wa Simba SC, Issa Batenga ataendelea kuwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, kufuatia kuteuliwa tena na Bodi ya Muda ya Wakurugenzi ya klabu hiyo Jumapili.
  Taarifa ya Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, imesema kwamba Bodi hiyo imeteua kamati ya uchaguzi ya watu watano kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo, chini ya Mwenyekiti, Boniphace Lyamwike na Makamu wake, Wakili Steven Ally.
  Issa Batenga anakuwa mtu pekee kutoka Kamati iliyopita ya Uchaguzi ya klabu hiyo kuwemo kwenye Kamati mpya na bahati nzuri anaendeleka na majukumu yale yale ya Ukatibu.
  Issa Batenga (kushoto) ataendelea kuwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC 

  Wajumbe wawili walioteuliwa kuungana na Lyamwike, Wakili Steven na Batenga ni Iddi Mbita na Richard Mwalwiba.
  Salim amesema kwamba Kamati hiyo itatangaza tarehe ya uchaguzi hivi karibuni na kuitisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simba SC (Simba Sports Club Company Limited) ambao watachaguliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 ya katiba ya klabu hiyo.
  Julai 24 mwaka huu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liliipa Simba siku 75 kuhakikisha inafanya uchaguzi wake kwani viongozi waliopo sasa wamemaliza muda.
  Kamati iliyopita ya Uchaguzi ya Simba SC iliundwa na Mwenyekiti Dk. Damas Daniel Ndumbaro, Makamu wake, Salum Madenge, Katibu Batenga, Katibu Msaidizi, Khalid Kamguna na Wajumbe Kassim Dewji, Juma Simba na Amin Bakhresa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BATENGA PEKEE AREJESHWA KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SC, MWENYEKITI MPYA LYAMWIKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top