• HABARI MPYA

  Saturday, August 18, 2018

  ALONSO AIFUNGIA LA USHINDI CHELSEA YAILAZA ARSENAL 3-2

  Marcos Alonso akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Chelsea dakika ya 81, akimalizia pasi ya Eden Hazard katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal Uwanja wa Stamford Bridge, London. Alonso alianza kumsetia Pedro kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya tisa kabla ya Alvaro Morata kufunga la pilio dakika ya 20, lakini Arsenal ikazinduka na kusawazisha yote kupitia kwa Henrikh Mkhitaryan dakika ya 37 na Alex Iwobi dakika ya 41. Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa kwa kocha Mspaniola, Unai Emery katika ligi tangu arithi mikoba ya kocha wa muda mrefu wa The Gunnes, Mfaransa Arsene Wenger 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALONSO AIFUNGIA LA USHINDI CHELSEA YAILAZA ARSENAL 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top