• HABARI MPYA

  Sunday, March 18, 2018

  SIMBA SC NA AL MASRY KATIKA PICHA JANA PORT SAID

  Mshambuliaji wa Al Masry, Mohamed Abdellatif 'Grendo' akitafuta maarifa ya kumpita beki Mghana wa Simba, Asante Kwasi katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Port Said, Misri. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0 na Al Masry inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam  
  Mohamed Abdellatif akimlamba chenga Asante Kwasi huku Mghana mwenzake, Asante Kwasi akishuhudia 
  Beki wa Simba, Mghana Asante Kwasi akiingiza mguu kuondoa mpira kwenye himaya ya mchezaji wa Al Masry, Mohamed Mostafa Emam 'Shatta'
  Mshambuliaji Mghana wa Simba, Nicholaus Gyan anayetumika kama beki katika mfumo wa sasa akimdhibiti winga wa Al Masry, Mohamed Ahmed 
   Ahmed Shokry wa Al Masry akipiga hesabu za kumpita beki wa Simba, Shomary Kapombe
  Beki wa Simba, YUssuf Mlipili akiokoa mbele ya mchezaji wa Al Masry jana 
  Kikosi cha Al Masry kabla ya mchezo wa jana Uwanja wa Port Said 
  Kikosi cha Simba kabla ya mchezo wa jana POrt Said
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA AL MASRY KATIKA PICHA JANA PORT SAID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top