• HABARI MPYA

  Sunday, March 18, 2018

  SAMATTA ASHINDWA KUINUA KOMBE LA UBELGIJI, GENK YAPIGWA 1-0 DAKIKA 120 BRUSSELSS

  Na Mwandishi Wetu, BRUSSELSS
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ameshindwa kuisaidia timu yake KRC Genk kutwaa Kombe kla Ubelgiji baada ya kufungwa 1-0 na Standard Liege katika mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Roi Baudouin mjini Brusselss.
  Samatta aliingia robo saa kabla ya filimbi ya mwisho kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake, Mgiriki, Nikolaos ‘Niko’ Karelis na akaenda kufanya jiihada ambazo hazikuzaa matunda.
  Wakati huo, timu hizo zilikuwa hazijafungana na zikamaliza dakika 90 kawaida zikiwa hazijapata bao kabla ya mchezo kuhamia kwenye nusu saa ya nyongeza.
  Mbwana Samatta akimtoka mchezaji wa Standard Liege jana mjini Brussells
  Mbwana Samatta akipiga shuti katika ya wachezaji wa Standard Liege jana mjini Brussells

  Shujaa wa alikuwa ni mshambuliaji Renaud Emond aliyefunga bao hilo pekee la ushindi wa mechi na Kombe lenyewe dakika ya 92 baada ya kazi nzuri ya Mbelgiji mwenzake, Mehdi Carcela-González.
  Jitihada zaidi za Samatta zikamuingiza kwenye orodha ya wachezaji 11 walioonyeshwa kadi za njano, baada ya kuonyeshwa kadi hiyo dakika ya 91 akiungana na Ndongala dakika ya 62 , Mpoku 66, Fai 81, Mata 82, Nastic 90, Marin 103, Carcela 105 sawa na Luyindama, Buffel 108 na Djenepo 116.
  Samatta jana amecheza mechi ya 79 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo, Mata, Seck, Malinovskyi/Wouters 110, Pozuelo, Ndongala/Trossard dk64, Buffalo na Karelis/Samatta dk73.
  Standard Liege: Gillet, Cimirot, Emond/Pocognoli dk121, Carcela/Djenepo dk105, Marin, Fai, Edmilson/Cop dk97, Koutroubis, Luyindama, Cavanda na Mpoku.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ASHINDWA KUINUA KOMBE LA UBELGIJI, GENK YAPIGWA 1-0 DAKIKA 120 BRUSSELSS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top