• HABARI MPYA

  Sunday, March 18, 2018

  NJOMBE MJI FC WAJIPANGA KUIPIGA STAND UNITED KULE KULE SHINYANGA KWAO ASFC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Njombe Mji FC umesema una imani na kocha wao, Ally Bushiri atawavusha katika Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Njombe itakuwa ugenini dhidi ya Stand United mchezo wa Robo Fainali ya ASFC unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Machi 30 mwaka huu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Katibu Mkuu wa Njombe Mji FC, Obedi Mwakasungula alisema kwamba wamekwishaweka mikakati ya kufanya vizuri katika mchezo huo huku wakiwa na imani na kocha huyo.
  Alisema kikosi chao kinaendelea vyema na mazoezi na maandalizi kwa ujumla na hakuna majeruhi hata mmoja.
  "Tangu amekuja kocha Bushiri tumeona mabadiliko kwenye timu yetu, pia hatuwezi kuwadharau Stand, ni timu nzuri imefanya mabadiliko kwa kuongeza nguvu benchi lake la ufundi kama ilivyo kwetu," alisema.
  Mwakisungula alisema malengo yao kuhakikisha wanasonga mbele katika michuano hiyo na wana imani na wachezaji wao wanaweza kuwafikisha pale wanapotarajia katika michuano hiyo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NJOMBE MJI FC WAJIPANGA KUIPIGA STAND UNITED KULE KULE SHINYANGA KWAO ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top