• HABARI MPYA

  Saturday, February 17, 2018

  YANGA SC YAENDA SHELISHELI BILA CHIRWA MAJERUHI, YATANGULIZA 'KACHERO' KUWEKA MIPANGO SAWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka kesho asubuhi mjini Dar es Salaam kwenda mjini Victoria kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns utakaofanyika siku ya Jumatano mjini humo.
  Lakini Msemaji wa Yanga SC, Dissmas Ten ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba katika kikosi hicho, mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Mzambia Obrey Chirwa hatakuwemo kutokana na kuwa majeruhi. 
  Pamoja na Chirwa, Ten amesema wote, Wazimbabwe kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma hawatakuwepo kwa sababu ya maumivu pia, wakati majeruhi wengine ni beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe ambao wote watakosekana pia.
  Obrey Chirwa atakosekana Yanga SC kwenye mchezo wa marudiano na Saint Louis nchiji Shelisheli 

  Samuel Lukumay (kushoto) yupo mjini Victoria, Shelisheli tangu Alhamisi kuandaa utaratibu wa timu itakapowasili 

  Kikosi cha kamili cha Yanga kinachiotarajiwa kuondoka kesho ni makipa; Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya na Youthe Rostand, mabeki Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Gardiel Michael, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Patto Ngonyani na Kelvin Yondani.
  Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Said Mussa, Emmanuel Martin, Geoffrey Mwashiuya n Juma Mahadhi, maana yake timu imekwenda bila mshambuliaji.
  Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Samuel Lukumay tayari yupo Victoria tangu Alhamisi kuandaa utaratibu wa timu itakapowasili katika kuhakikisha wanafikia kwenye mazingira salama na kuepuka hujuma za wenyeji kuelekea mchezo huo, ambao wanahitaji kuulinda ushindi wao mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  Lukumay amekwishaandaa mazingira ya timu kufikia mjini kuanzia hoteli ya kuishi, chakula salama hadi Uwanja wa kufanyia mazoezi. Na kwa miaka ya karibuni, Lukumay ndiye amekuwa akitangulizwa na Yanga ugenini kufanya kazi hiyo na kwa kiasi kikubwa amekuwa akiifanya vizuri.
  Yanga wanahitaji kuulinda ushindi wao mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAENDA SHELISHELI BILA CHIRWA MAJERUHI, YATANGULIZA 'KACHERO' KUWEKA MIPANGO SAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top