• HABARI MPYA

  Tuesday, February 13, 2018

  TIMU YA SAMATTA YALIMWA FAINI KWA KUTOINGIA VYUMBANI MECHI WALIYOPANDA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya African Lyon imepigwa faini ya Sh. 200,000, kutokana na kutoingia vyumbani katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya Kiluvya United iliyofanyika Februari 5 Uwanja wa Filbert Bayi mkoani Pwani.
  Katikati mechi hiyo ambayo Lyon, timu ya zamani ya mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ilishinda 1-0 na kupanda Ligi Kuu, imedaiwa kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(13) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo. 
  Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Mbwana Samatta aliibukia African Lyon (kulia) na sasa anacheza Ulaya 

  Mechi namba 53 Kundi B (Mawenzi Market 0 v Coastal Union 2). Klabu ya Mawenzi Market imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuwarushia chupa Waheshimiwa Mawaziri ambao ni washabiki wa Coastal Union katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 2, 2018 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Adhabu dhidi ya klabu ya Mawenzi Market imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
  Mechi namba 53 Kundi C (Alliance Schools 2 vs JKT Oljoro 1). Wachezaji Ramadhani Yego na Joseph Mkota wa JKT Oljoro wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutaka kumpiga Mwamuzi baada ya kumalizika mechi hiyo iliyochezwa Februari 4, 2018 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
  Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF ilikutana Jumamosi Februari 10, 2018 kupitia mashauri yaliyofikishwa kwenye kamati hiyo.
  Shauri namba moja lilihusisha malalamiko dhidi ya wachezaji Saba(7) wa timu ya Transit Camp,shauri ambalo lilihudhuriwa na mchezaji mmoja Mohamed Suleiman Ussi.
  Mchezaji Mohamed Suleiman Ussi alituhumiwa kwa kosa la utovu wa nidhamu kwenye mechi namba 48 ya Kundi C Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara akidaiwa kutaka kumpiga Mwamuzi wa mchezo kinyume na Ibara ya 50(1)(2) na (5)ya Katiba ya TFF toleo la 2015.
  Kamati ilipitia ripoti ya kamishna wa mechi ambayo pamoja na kuwataja wachezaji wengine wengine pia ilimtaja Mohamned Suleiman Ussi kuhusika kwenye tukio hilo akiwa amevaa jezi namba 14 ambaye pia alitajwa kwenye ripoti ya mwamuzi ikielezea kitendo cha Mohamed Suleiman Ussi kutaka kumpiga mwamuzi msaidizi namba 2.
  Baada ya kupitia ripoti Kamati imejiridhisha kuwa mchezaji Mohamed Suleiman Ussi alitaka kumpiga mwamuzi kinyume na kanuni ya 36 ya Ligi Daraja la Kwanza  na ibara ya 50(1)(2) na (5) ya Katiba ya TFF toleo la 2015.
  Kamati imemuadhibu Mohamed Suleiman Ussi imemfungia kutocheza michezo mitatu(3) pamoja na faini ya Shilingi laki tatu(300,000) kwa mujibu wa kanuni ya 37(7) na 37(12) kanuni za Ligi Daraja la Kwanza.
  Kilimanjaro Heroes imepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ya Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara dhidi ya Pepsi iliyofanyika Februari 3, mwaka huu Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, ambayo ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) taratibu za mchezo.
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kilichofanyika mjini Dar es Salaam.
  Adhabu dhidi ya Kilimanjaro Heroes imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Mechi namba 30 Kundi B (African Sports 2 v AFC 0). Wachezaji wa AFC, John George Rasta na Shaibu Salim wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutaka kumshambulia Mwamuzi kabla ya kuokolewa na viongozi wa timu hiyo katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
  Klabu ya AFC imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA SAMATTA YALIMWA FAINI KWA KUTOINGIA VYUMBANI MECHI WALIYOPANDA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top