• HABARI MPYA

  Tuesday, December 19, 2017

  FIFA YAIFUNGULIA TENA TANZANIA MTANDAO WA USAJILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE Mfumo wa Usajili wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa njia ya mtandao, maarufu kama TMS umefunguliwa tena kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom na Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
  Hiyo inafuatia kurekebishwa kwa hitilafu zilizojitokeza baada ya jitihada za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwasiliana na waendeshaji wa mfumo huo  walioko Tunis, Tunisia ili kuziwezesha timu za Bara ziendelee na usajili.
  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba mtandao huo kwa sasa upo wazi. “Hivyo TFF inazitaka timu zote sasa kukamilisha usajili kuanzia pale walipokwama. Timu zinatakiwa kusajili kabla ya Desemba 23, mwaka huu,” amesema Lucas.
  Desemba 15, mwaka huu mfumo wa usajili kwa njia ya TMS ulifeli hali iliyosababisha vilabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.
  Katika mawasiliano na kampuni hiyo, FIFA na CAF wamekuwa wakipewa Taarifa ya kila hatua inayochukuliwa na TFF hadi mfumo huo kufunguka leo Desemba 19, 2017.
  Bado TFF inasisitiza vilabu vyote kuzingatia kusajili kwa wakati pale inapotokea dirisha la usajili limefunguliwa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YAIFUNGULIA TENA TANZANIA MTANDAO WA USAJILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top