• HABARI MPYA

    Tuesday, October 10, 2017

    TFF YAZIONYA BULYANHULU, MKAMBA RANGERS NA REHA, YAMFUNGIA ALIYEMPIGA REFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imetoa onyo kali kwa klabu za Bulyanhulu FC, Mkamba Rangers bna Reha katika kikao chake kilichopita cha kupitia taarifa na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2017/2018 zinazoendelea hivi sasa.
    Katika taarifa hizo imebainika kuwa timu Bulyanhulu haikuhudhuria katika kikao cha maandalizi (pre match meeting) wakati wa mechi namba 3 ya Kundi D dhidi ya Milambo FC iliyochezwa Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
    Kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Daraja la Pili. Kwa vile ni kosa la kwanza kwa timu yako msimu huu, Kamati imeipa klabu hiyo Onyo Kali kwa kuamini kuwa kosa hilo la kikanuni halitajitokeza tena. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
    Mkamba Rangers imepewa onyo kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi (pre match meeting), na pia ilichelewa kufika uwanjani wakati wa mechi namba 3 ya Kundi C dhidi ya Boma FC iliyochezwa Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Mwakangale uliopo Kyela mkoani Mbeya.
    Kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) na Kanuni ya 14(9) za Ligi Daraja la Pili. Kwa vile ni kosa la kwanza kwa timu yako msimu huu, Kamati imeipa klabu yako Onyo Kali kwa kuamini kuwa kosa hilo la kikanuni halitajitokeza tena. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) na 14 (48) za Ligi Daraja la Pili.
    Reha imeonywa kwa kuwakilishwa na viongozi watatu tu katika kikao cha maandalizi (pre match meeting) wakati wa mechi namba 3 ya Kundi A dhidi ya Namungo FC iliyochezwa Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
    Kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Pili. Kwa vile ni kosa la kwanza kwa timu yako msimu huu, Kamati imeipa klabu yako Onyo Kali kwa kuamini kuwa kosa hilo la kikanuni halitajitokeza tena. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
    Kamati imezikumbusha klabu zote, kuwa Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zinaendeshwa kwa kuzingatia Kanuni husika, hivyo watendaji wakuu wa klabu wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kanuni hizo zinafuatwa kikamilifu.
    Katika hatua nyingine, Kamati imemsimamisha John Baraka kucheza mechi za SDL hadi suala lake litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Kamati imechukua hatua hiyo kwa kwa kutumia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi. 
    Kamati imebainika Baraka anayevaa jezi namba mbili, alioneshwa kadi nyekundu baada ya mchezo kumalizika kwa kumpiga mwamuzi ngumi ya mgongoni kwenye mechi namba 1 ya Kundi D la Ligi Daraja la Pili kati ya timu yako na Nyanza FC iliyofanyika Oktoba 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyerere uliopo Mbulu mkoani Pwani. 
    Mchezaji huyo atafahamishwa siku ambayo kikao cha Kamati ya Nidhamu kitafanyika kusikiliza shauri dhidi yake ambapo pia atapata fursa ya kuwasilisha utetezi wake kama upo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAZIONYA BULYANHULU, MKAMBA RANGERS NA REHA, YAMFUNGIA ALIYEMPIGA REFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top