• HABARI MPYA

    Tuesday, May 02, 2017

    SERENGETI BOYS YABADILISHIWA KITUO GABON, YAPELEKWA LIBREVILLE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys, imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa Libreville.
    Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon, litakuwa Port Gentil.
    Kwa sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yauonde.
    Wenyeji hao, Cameroon watarudiana na Serengeti Boys katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kesho Jumatano, Mei 3, mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YABADILISHIWA KITUO GABON, YAPELEKWA LIBREVILLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top