• HABARI MPYA

    Friday, May 05, 2017

    MAN CITY YAFUNGIWA MIAKA MIWILI KUSAJILI ENGLAND

    KLABU ya Manchester City imefungiwa kwa miaka miwili kusajili wachezaji wa umri chini ya miaka 18 sambamba na kutozwa faini ya Pauni 300,000 na Bodi ya Ligi Kuu England kwa kuvunja sheria ya maendeleo ya vijana.
    Uvunjaji huo wa sheria unahusu kufanya mazungumzo na wachezaji wawili wa akademi tofauti kwa ajili ya kuwasajili huku wakiwa wamesajiliwa na klabu nyingine. 
    Adhabu hiyo ni sawa na waliyopewa Liverpool mwezi uliopita baada ya kukutwa na hatia ya 'kuiba' mchezaji mwanafunzi wa shule wa Stoke City.
    Kufuatia uchunguzi wa Bodi ya Ligi Kuu, ushahidi umepatikana kwa City ambao wamevunja sheria za Ligi.
    Kuwasilia na mchezaji wa akademi yoyote akiwa amesajiliwa na klabu yake ya wakati husika ni kosa, ambalo City wamefanya na sasa linawagharimu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YAFUNGIWA MIAKA MIWILI KUSAJILI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top