• HABARI MPYA

  Wednesday, May 03, 2017

  HIMID MAO ATUA LIGI KUU DENMARK KWA MAJARIBIO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Azam FC, Himid Mao Mkami yupo nchini Denmark tangu jana kwa ajili ya majaribio ya kujiunga na klabu ya Randers FC ya Ligi Kuu.
  Timu hiyo yenye maskani yake mjini Randers, imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu Himid na kurudishiwa na uwezo wake kabla ya kumualika kwa majaribio ili kujiridhisha zaidi.
  Taarifa zinasema ni mambo madogo tu Randera FC inayofundishwa na Olafur Kristjsnsson inataka kutazama katika majaribio ya Himid kabla ya kumpa mkataba.
  Himid Mao Mkami yupo nchini Denmark kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Randers FC ya Ligi Kuu

  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana usiku, Himid alisema kwamba  anamshukuru Mungu amefika salama na sasa anajipanga kuanza majaribio yake.
  “Hii ni nafasi muhimu kwangu, baada ya kucheza kwa muda mrefu Azam FC sasa ni wakati mwafaka kutoka nje, naomba Mungu anisaidie nifanye vizuri katika majaribio yangu,”alisema Himid.
  Mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Mao Mkami ‘Ball Dancer’ pamoja na kufanya mazoezi na Rabnders kuanzia jana, pia anatarajiwa kuwa jukwaani wakati timu hiyo ikimenyaa na AC Horsens Jumanne ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO ATUA LIGI KUU DENMARK KWA MAJARIBIO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top