• HABARI MPYA

  Friday, May 05, 2017

  EURO MILIONI 14 KWA MSIMU ZAMSUBIRI AUBAMEYANG PSG

  TIMU ya Paris Saint-Germain inataka kuweka dau la Euro Milioni 70 kwa Borussia Dortmund ili wamnunue mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.
  Taarifa kutoka ndani ya PSG zinakanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Bild la Ujerumani kwamba mzaliwa huyo wa Ufaransa, ambaye amefunga mabao 35 msimu huu, tayari amekutana na Mkurugenzi wa Soka wa PSG, Patrick Kluivert mjini Paris.
  Aubameyang, mwenye umri wa miaka 27, atakuwa anaingiza Euro Milioni 14 kwa msimu akitua PSG, pato ambalo ni mara mbili ya mshahara wake wa sasa.
  Mshahara wa Euro Milioni 14 kwa msimu unamsubiri  Pierre-Emerick Aubameyang akitua PSG 

  Dortmund inajipanga kupokea ofa ya PSG msimu utakapomalizika baada ya fainali ya Kombe la Ujerumani Mei 27 dhidi ya Eintracht Frankfurt, taarifa zimesema.
  Lakini mzaliwa huyo wa Ufaransa raia wa Gabon, amekuwa akirudia kusema kwamba anataka kujiunga na Real Madrid au angalau kucheza Ligi ya Hispania, ingawa famili yake ipo Paris.
  Mshambuliaji huyo amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake Dortmund, lakini imedokezwa anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu na klabu hiyo ya Ujerumani haijakataa kumuuza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EURO MILIONI 14 KWA MSIMU ZAMSUBIRI AUBAMEYANG PSG Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top