• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2017

  ZULU NJE WIKI MBILI BAADA YA PIGO LA KININJA LA HIMID LEO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Yanga, Mzambia Justin Zulu anatarajiwa kuwa nje kwa kipindi kisichopungua wiki mbili, kufuatia kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mchezaji huyo wa zamani wa Zesco United ya kwao, Zambia aliwekewa guu na kiungo wa Azam, Himid Mao Mkami wakati anapiga shuti jioni ya leo na kuumia vibaya kiasi cha kuchanika nyama za ugoko, hivyo kushindwa kuendelea na mchezo huo, akimpisha Emmanuel Martin dakika ya 30.
  Moja kwa moja Zulu aliyewahi pia kuchezea timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ alienda kutibiwa kwenye zahanati ndogo ya Uwanja Taifa, ambako alishonwa nyuzi tisa chini ya Daktari Nassor Matuzya.
  Justin Zulu akitibiwa na Dk Nassor Matuzya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
  Hivi ndivyo ambavyo Justin Zulu ameumia baada ya rafu ya Himid Mao

  Justin Zulu akitibiwa na Dk Nassor Matuzya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Ni Daktari huyo wa tiba za wanamichezo, Matuzya aliyesema kwamba Zulu atakuwa nje kwa muda usiopungia wiki mbili.
  “Atakaa na nyuzi kwa muda wa wiki moja na baada ya hapo itahitaji wiki moja kumpa muda jeraha lake kupona vizuri, kutoka hapo anaweza kuanza mazoezi mepesi,”alisema Dk Matuzya.
  Hii ni mara ya pili kwa Himid, maarufu kwa jina la utani Ninja kumuweka nje muda mrefu Zulu baada ya kumchezea rafu, kufuatia Januari mwaka huu kumfanyia hivyo pia kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi na Mzambia huyo aliyekuwa ndiyo kwanza anajiunga na Yanga mwezi huo akakaa nje wiki tatu.    
  Aidha, kuumia kwa mchezaji huyo kunaongeza idadi ya majeruhi Yanga iliyoshinda 1-0 leo bao pekee la Mzambia, Obrey Chirwa na kufika wanne, akiungana na Wazimbabwe kiungo Thabani Kamusoko, washambuliaji Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZULU NJE WIKI MBILI BAADA YA PIGO LA KININJA LA HIMID LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top