• HABARI MPYA

  Wednesday, February 01, 2017

  SAMATTA AUMIA DAKIKA YA 23, GENK YACHAPWA NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alicheza kwa dakika 23 tu kabla ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo akiiacha timu yake, KRC Genk ikifungwa 1-0 na KV Oostende Uwanja Luminus Arena, Genk katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji na kutolewa.
  Samatta aliumia dakika ya 23 na kulazimika kumpisha Mspaniola Jose Naranjo ambaye alikwenda kukosa penalti na bao la Mzimbabwe, Knowledge Musona dakika ya nane likaimaliza Genk.
  Mbwana Samatta akirudi benchi baada ya kuumia jana KRC Genk ikifungwa 1-0 na KV Oostende 

  Huo ni mchezo wa pili mfululizo KRC Genk inapoteza, baada ya mwishoni mwa wiki kuchapwa 1-0 na KV Mechelen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji. 
  Siku hiyo Samatta alicheza kwa dakika zote 90 jana Uwanja wa ugenini wa AFAS Achter de Kazerne mjini Mechelen na bao pekee la beki Mbelgiji, Seth De Witte dakika ya 89 likawapa wenyeji ushindi wa 1-0.
  Jana Samatta amecheza mechi ya 40 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 22 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 21 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 10 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 11, matano msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi KRC Genk kilikuwa: Ryan, Uronen, Colley, Dewaest/Susic dk72 Castagne, Heynen, Malinovskyi/Berge dk85, Pozuelo, Trossard, Authors na Samatta/Naranjo dk23.
  KV Oostende: Dutoit, El Ghanassy, Berrier/Canesin dk88 Musona/Jali dk86, Rozehnal, Dimata/Akpala dk74, Jonckheere, Vandendriessche, Capon, Godeau na Milic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AUMIA DAKIKA YA 23, GENK YACHAPWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top