• HABARI MPYA

    Wednesday, February 22, 2017

    KASEJA MCHEZAJI BORA WA JANUARI LIGI KUU YA VODACOM

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA wa Kagera Sugar, Juma Kaseja Juma amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Januari kwa msimu wa 2016/2017.
    Kaseja aliwashinda wachezaji Mbaraka Abeid pia wa Kagera Sugar na Jamal S. Mtengeta wa Toto African.
    Katika mechi tatu ambazo timu ya Kagera ilicheza kwa mwezi huo, Kaseja ambaye alicheza kwa dakika zote 270 alikuwa kiongozi na mhimili wa timu na aliisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo yote ambapo ilikusanya jumla ya pointi 9 zilizoifanya timu hiyo kupanda nafasi mbili katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo wa Januari (kutoka nafasi ya 5 hadi ya 3).
    Katika michezo hiyo mitatu, Kagera Sugar ilifunga mabao sita na Kaseja alifungwa bao moja tu na alionesha nidhamu ya hali ya juu ikiwemo kutopata onyo lolote (kadi).
    Kwa kushinda tuzo hiyo, Kaseja atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEJA MCHEZAJI BORA WA JANUARI LIGI KUU YA VODACOM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top