• HABARI MPYA

    Monday, February 27, 2017

    NNE BORA YA LIGI DARAJA LA PILI KUANZA JUMATANO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU nne vinara wa Ligi Daraja la Pili kutoka makundi manne, zinatarajiwa kuanza kupambana keshokutwa Jumatano - Machi mosi, mwaka huu ‘Play off’ kutafuta timu Tatu Bora, zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2017/2018.
    Timu hizo zilizofanya vema ni pamoja na JKT Oljoro ya Arusha, Cosmopolitan ya Dar es Salaam, Mawenzi ya Morogoro na Transit Camp ya Shinyanga. Ziliibuka vinara katika makundi yao.
    Ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi, inaonesha kuwa Ratiba ya Nne Bora itakuwa na raundi mbili ambazo kwa pamoja zitacheza kwa mwezi mmoja kuanzia Machi mosi hadi Aprili mosi, mwaka huu.
    Raundi ya kwanza itaanza siku ya Machi mosi, mwaka huu ambako kutakuwa na mechi mbili ambazo Transit Camp itacheza na Mawenzi kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati Cosmopolitan itacheza na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Machi 5, mwaka huu kutakuwa pia na michezo miwili ambako JKT Oljoro itacheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Mawenzi Market itacheza Cosmopolitan kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
    Machi 12, mwaka huu JKT Oljoro itacheza na Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Cosmopolitan itacheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Raundi ya Pili ya ligi hiyo, itaanza Machi 18, mwaka huu kwa timu za Mawenzi Market itacheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati siku hiyo, JKT Oljoro itacheza na Cosmopolitan katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
    Machi 25, mwaka huu Cosmopolitan itapambana na Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam ilihali Transit Camp itacheza na JKT Oljoro Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
    Funga dimba la hatua hiyo, itakuwa Aprili mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako Mawenzi itakuwa mwenyeji wa JKT Oljoro wakati Cosmopolitan itakuwa mgeni wa Transit Camp kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NNE BORA YA LIGI DARAJA LA PILI KUANZA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top