• HABARI MPYA

    Monday, February 27, 2017

    TFF YAUFUNGULIA UWANJA WA JAMHURI, YANGA NA MTIBWA MACHI 5

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limerejesha tena mechi za Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Jumapili Machi 5, mwaka huu Mtibwa Sugar itaialika Yanga kwenye uwanja huo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Ikumbukwe TFF iliufungia Uwanja wa Jamhuri ili kutoa fursa kwa wamiliki wake kuufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea mpira na pia askari polisi kupata maelekezo ya kutosha ya jinsi ya kusimamia usalama uwanjani badala ya kutazama mechi. 
    Hatua hiyo ilifuatia mashabiki kuingia uwanjani baada ya mechi namba 151 baina ya wenyeji, Mtibwa Sugar na Simba Januari 18, mwaka huu. 
    TFF ilisema baada ya mchezo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari na kamera ya Azam Tv upande wa goli la Kusini iliangushwa na washabiki hao.
    Vilevile sehemu ya kuchezea (pitch) ya Uwanja wa Jamhuri ilikuwa katika hali mbaya iliyohitaji marekebisho makubwa ili iweze kuendelea kutumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAUFUNGULIA UWANJA WA JAMHURI, YANGA NA MTIBWA MACHI 5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top