• HABARI MPYA

    Monday, February 20, 2017

    KOCHA AMAJITA ATAJA KIKOSI CHA UBINGWA AFCON U-20 ZAMBIA 2017

    KOCHA wa timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini chini ya umri wa miaka 20, Thabo Senong ametaja kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 (u20 Afcon) zitakazofanyika Zambia kuanzia Februari 26 hadi Machi 12 mwaka huu.
    Zikiwa imebaki wiki moja kuanza michuano hiyo, Senong amesema kikosi cha Amajita kina ubora wa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
    Amajita imepangwa Kundi B, sambamba na Senegal, Cameroon na Sudan na watacheza mechi zao mjini Ndola wakati Kundi A mechi zake zitachezwa Lusaka, likihusisha timu za wenyeji, Zambia, Misri, Mali na Guinea. 
    Timu nne za juu zitafuzu moja kwa moja kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2017 nchini Korea Kusini kuanzia Mei 20 hadi Juni 11.
    Kikosi cha Amajita kinaundwa na makipa; Sanele Tshabalala wa Bidvest Wits F.C, Mondli Mpoto wa SuperSport United na Kubheka wa Mamelodi Sundowns F.C.
    Mabeki ni Notha Ngcobo wa Mamelodi Sundowns, Tercious Malepe wa Orlando Pirates F.C, Aghmat Ceres wa Ajax Cape Town F.C, Siyabonga Ngezana wa Kaizer Chiefs F.C, Katlego Mohamme wa SuperSport United F.C, Sandile Mthethwa wa Orlando Pirates F.C na Thendo Mukumela wa Mamelodi Sundowns F.C.
    Viungo ni Teboho Mokoena wa SuperSport United F.C, Sipho Mbule wa Orlando Pirates F.C, Wiseman Meyiwa wa Kaizer Chiefs F.C, Phakamani Mahlambi wa Bidvest Wits F.C, Sibongakonke Mbatha wa Bidvest Wits F.C, Kobamelo Kodisang wa Platinum Stars F.C na Grant Margeman wa Ajax Cape Town F.C.
    Washambuliaji ni Itumeleng Shopane wa Kaizer Chiefs F.C, Khanyisa Mayo wa SuperSport United F.C, Liam Jordan wa Sporting CP (Ureno), Luther Singh wa Sporting Braga B (Ureno).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA AMAJITA ATAJA KIKOSI CHA UBINGWA AFCON U-20 ZAMBIA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top