• HABARI MPYA

  Monday, October 14, 2019

  SENEGAL WAIGONGA GHANA KWA PENALTI NA KUTWAA KOMBE LA WAFU

  SENEGAL 'Simba wa Teranga' imefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Magharibi mwa Afrika (WAFU) baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Ghana 'Black Stars' jana Uwanja wa Lat Dior mjini Thies.
  Youssouph Mamadou Badji aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 107 nyongeza kufuatia kutokea benchi kabla ya Joseph Esso kuisawazishia Ghana dakika ya 109 na mchezo ukahamia kwenye matuta.
  Kipa wa Generation Foot ya Senegal, Pape Saidou Ndiaye ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuokoa penalti mbili, ya Justice Blay na Augustine Okrah wakati Mohammed Fatau akagongesha mwamba mkwaju wake kuwapa weneji taji la WAFU.

  Senegal waliianaa michuano kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Guinea-Bissau, kabla ya kuichapa Benin 1-0 kwenye Robo Fainali na kushinda 2-0 dhidi ya Mali kwenye Nusu Fainali.
  Ghana waliingia kwenye mashindano haya kama mabingwa watetezi, baada ya mafanikio yao ya mwaka 2017 katika ardhi ya nyumbani pia. 
  Walianza na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Gambia kabla ya kuzitoa pia Burkina Faso na Ivory Coast katika Robo Fainali na Nusu Fainali.
  Fainali ya Plate pia iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti, Guinea ikiifunga Cape Verde baada ya sare ya 0-0.
  Nyota wa Guinea, Jean Mouste ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano, wakati Mfungaji Bora ni Mumuni Shafiu wa Ghana na Kipa Bora ni Alpha Jalloh wa Liberia.
  Nigeria watakuwa wenyeji wa fainali zijazo za WAFU mwaka 2021.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SENEGAL WAIGONGA GHANA KWA PENALTI NA KUTWAA KOMBE LA WAFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top