• HABARI MPYA

    Thursday, October 24, 2019

    KILIMANJARO QUEENS YAPANGWA NA ZANZIBAR, BURUNDI NA SUDAN KUSINI CECAFA CHALELENGE WANAWAKE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WENYEJI, Tanzania Bara wamepangwa Kundi A pamoja na ndugu zao, Zanzibar, Burundi na Sudan Kusini katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Chalelenge wanawake) inayotarajiwa kuanza Novemba 14 hadi 24 mjini Dar es Salaam.
    Kundi B linaundwa na timu za Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibouti na Kilimanjaro Queens ambao pia ndio mabingwa watetezi watafungua dimba na Sudan Kusini Novemba 14, kabla ya kumenyana na Burundi Novemba 16 na kukamilisha mechi zao za Kundi A kwa kumenyana na Zanzibar Novemba 18.

    Mechi zote za mashindano hayo zitafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam ambao unamilikiwa na klabu ya Azam FC, mali ya mfanyabiashara Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
    Kikosi cha Kilimanjaro Queens kilicho chini ya kocha Bakari Nyundo Shime, anayesaidiwa na Edna Lema kinaendelea na mazoezi yake mjini Dar es Salaam.
    Challenge ya wanawake itafanyika kwa mara ya tatu tu kihistoria mwaka huu baada ya 2016 Jinja nchini Uganda na 2018 mjini Kigali, Rwanda mara zote Kilimanjaro Queens wakibeba taji hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAPANGWA NA ZANZIBAR, BURUNDI NA SUDAN KUSINI CECAFA CHALELENGE WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top