• HABARI MPYA

    Tuesday, October 22, 2019

    YANGA SC YAWAPIGA MBAO FC 1-0 BAO PEKEE LA SADNEY URIKHOB MECHI YA LIGI KUU MWANZA

    Na Mwandishi Wetu, MWANZA
    YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Mbao FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
    Shukrani kwa bao pekee la mshambuliaji kutoka Namibia, Sadney Urikhob Khoetge dakika ya 57 akimalizia krosi ya kiungo, Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’ kutoka upande wa kushoto.
    Kwa ushindi huo wa pili mfululizo kwenye Ligi Kuu baada ya kuichapa na Coastal Union ya Tanga 1-0 pia kwenye mechi iliyopita, Yanga SC inafikisha pointi saba katika mchezo wa nne, nyingine mbili wakifungwa 1-0 na Ruvu Shooting na kutoa sare ya 3-3 na Polisi Tanzania, zote Dar es Salaam.


    Refa Meshack Suda wa Singida aliyesaidiwa na Athumani Rajab na Soud Hussein wote wa Kigoma alikataa bao la kila timu kipindi cha kwanza kutokana na wafungaji wote kukwamisha mpira nyavuni wakiwa wamezidi.
    Alianza Yusssuf Athumani wa Mbao FC kuukwamisha mpira nyuma ya kipa Mkenya Faroukh Shikalo dakika ya 37, kabla ya mshambuliaji David Molinga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), naye kutia mpira nyavuni dakika ya 41. 
    Lakini kipindi cha pili mambo yakaenda vizuri kwa Yanga SC wakifanikiwa kupata bao bao lao pekee la ushindi.
    Yanga inarejea kambini kuendelea na maandalizi ya mchezo wake wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pryramids FC ya Misri utakaofanyika Jumapili wiki hii hapo hapo Kirumba.
    Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Abdallah Makangana, Datius Peter, Emanuel Charles, Abdulrahman Said, Babilas Chitembe, Chilo Mkama/ Kauswa Benard dk65, Mussa Haji Gabi, Rajab Rashid, Said Junior, Yusssuf Athumani/ Jordan John dk42 na Adili Sultan/ Wazir Junior dk63.
    Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Ali Mtoni, Ali Hamad Ali, Kelvin Yondan, Feisal Salum/ Abdulaziz Makame dk77, Mapinduzi Balama, Papy Kabamba Tshishimbi, David Molinga/ Juma Balinya dk77, Sadney Urikhob na Mrisho Ngassa/Patrick Sibomana dk85.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAWAPIGA MBAO FC 1-0 BAO PEKEE LA SADNEY URIKHOB MECHI YA LIGI KUU MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top