• HABARI MPYA

    Wednesday, October 16, 2019

    MVUA YATIBUA MCHEZO WA KIRAFIKI YANGA SC NA PAN AFRICANS LEO JIONI UWANJA WA UHURU

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    MCHEZO wa kirafiki baina ya Yanga SC na Pan Africans umeshindwa kufanyika kutokana na maji kujaa Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo baada ya mvua iliyonyeshea kutwa kuanzia mchana.
    Yanga SC ilitaka kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Pyramids FC ya Misri wiki ijayo mjini Mwanza.
    Sasa Yanga watakuwa na mchezo mmoja tu zaidi kabla ya kuwavaa Pyramids FC ambao ni wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Jumanne ya wiki ijayo.

    Na ni hapo hapo Kirumba Yanga watakuwa wenyeji wa Pyramids FC Jumapili ya Oktoba 27, mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Bado Pyramids FC hawajataja rasmi Uwanja utakaotumika kwa mchezo wa marudiano Novemba 3, mwaka huu ingawa inafahamika wamekuwa wakitumia Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo kwa mechi zao za nyumbani.
    Yanga imeangukia katika mchujo baada ya kutolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 Ndola. 
    Katika Raundi ya kwanza, Yanga iliitoa Township Rollers ya Botswana kwa mabao 2-1, ikishinda 1-0 Gaborone baada ya sare ya 1-1 Dar es Salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MVUA YATIBUA MCHEZO WA KIRAFIKI YANGA SC NA PAN AFRICANS LEO JIONI UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top