• HABARI MPYA

  Saturday, August 03, 2019

  TANZANITE YAANZA VYEMA MICHUANO YA COSAFA, YAICHAPA BOTSWANA 2-0

  Na Mwandishi Wetu, PORT ELIZABETH
  TIMU ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeanza vyema michuano ya COSAFA baada ya kuichapa 2-0 Botswana Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini Ijumaa.
  Mabao ya Tanzanite inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime yamefungwa na Opa Clement dakika ya 38 na Klaotswe aliyejifunga dakika ya 48.  
  Katika mchezo huo, mchezaji wa Tanzanite, Diana Msemwa alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Tanzanite inayofundishwa na Bakari Shime itateremka tena dimbani kesho kumenyana na Eswatini, kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Zambia Jumanne.


  Kundi A linaundwa na wenyeji, Afrika Kusini, Namibia, Msumbiji na Zimbabwe na michuano hiyo iliyoanza juzi, itafikia tamati Agosti 11 mjini Port Elizabeth.
  Diana Msemwa akikabidhiwa tuzo ya Mchezaji bora wa mechi dhidi ya Botswana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YAANZA VYEMA MICHUANO YA COSAFA, YAICHAPA BOTSWANA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top