• HABARI MPYA

    Tuesday, August 20, 2019

    YANGA SC WANA MATUMAINI MAKUBWA YA KUWAMALIZA TOWNSHIP ROLLERS KWAO

    Na Mwandishi Wetu, GABORONE
    MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela amesema kwamba wachezaji wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Township Rollers Jumamosi Uwanja wa Taifa wa Gaborone.
    Akizungumza mjini hapa leo, Mwakalebela amesema kwamba kikosi kimefikia katika hoteli ya Crystal Palace mjini hapa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Shirikisho la Soka Botswana ambao ni wa nyasi bandia.
    “Tunafanya mazoezi kwenye Uwanja wa FA ya huku ambao ni wa nyasi bandia na ni mzuri kabisa na wachezaji wanafirahia. Kwa ujumla wachezaji wana ari kubwa kuelekea mechi hii,”amesema Mwakalebala ambaye pia ni Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


    Wachezaji wa Yanga SC baada ya kuwasili mjini Gaborone tayari kwa mchezo na wenyei, Township Rollers Jumamosi 

    Yanga SC inahitaji ushindi wa ugenini lazima ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo, kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani, Jumamosi na Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
    Baada ya mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, Yanga iliweka kambi ya wiki moja mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambako hali yake ya hewa inakaribia kufanana na ya Botswana.
    Na ikiwa huko ilicheza mechi mbili za kujipima nguvu, ikifungwa moja 2-0 na wenyeji, Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi na kushinda moja, 1-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WANA MATUMAINI MAKUBWA YA KUWAMALIZA TOWNSHIP ROLLERS KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top