• HABARI MPYA

  Saturday, August 31, 2019

  BARCELONA YABANWA, YATOA SARE YA 2-2 NA OSASUNA LA LIGA

  KINDA wa umri wa miaka 16, winga wa Guinea-Bissau, Anssumane 'Ansu' Fati akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kusawazisha dakika ya 51 akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya or Nelson Semedo katika sare ya 2-2 na wenyeji, Osasuna Uwanja wa El Sadar. Mabao yote ya Osasuna yamefungwa na Roberto Torres dakika ya saba na 81 kwa penalti, wakati bao lingine la Barcelona limefungwa na Arthur dakika ya   
  64. Winga huyo wa Guinea-Bissau, Fati mwenye umri wa miaka 16 na siku 304, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu mdogo kufunga bao kwenye historia ya miaka 90 ya La Liga baada ya Fabrice Olinga aliyeifungia Malaga akiwa na miaka 16 na siku 98 na Iker Muniain aliyekuwa na miaka 16  na siku 289 alipoichezea kwa mara ya kwanza Athletic Bilbao 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YABANWA, YATOA SARE YA 2-2 NA OSASUNA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top