• HABARI MPYA

    Saturday, August 24, 2019

    KAGERA SUGAR, NAMUNGO, POLISI ZAANZA VYEMA LIGI KUU, MBEYA CITY NA PRISONS 0-0

    MATOKEO TOTE MECHI ZA LIGI KUU LEO
    Kagera Sugar 2-0 Biashara United
    Polisi Tanzania 1-0 Coastal Union
    Mbeya City 0-0 Tanzania Prisons
    Mbao FC 1-1 Alliance FC
    Namungo 2-1 Ndanda FC
    MECHI ZA KESHO
    Mwadui FC V Singida United Saa 10:00 Jioni
    Lipuli FC V Mtibwa Sugar Saa 10:00 Jioni

    Na Mwandishi Wetu, MUSOMA
    TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imeanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara jioni ya leo. 
    Mabao ya Kagera Sugar inayofundishwa na beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania leo yamefungwa na Yussuf Mhilu dakika ya 14 na Awesu Awesu dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao wenyeji walikosa penalti iliyopigwa na Jarome Lambere.
    Mechi za Ligi Kuu leo, bao pekee la Mohamed Mkopi dakika ya 33 liliwapa ushindi wa 1-0 Polisi Tanzania dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati Mbeya City imetoa sare ya 0-0 na mahasimu wao wa Jiji, Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Nayo Mbao FC ililazimishwa sare ya 1-1 na wapinzani wao wa Jiji, Alliance FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Mbao FC walitangulia kwa bao la Paschal Frank dakika ya 28, kabla ya Ibrahim Said kujifunga dakika ya 90 na ushei kuipa Alliance bao la kusawazisha.
    Nayo Namungo FC ikaanza vyema kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mabao yake yote yakifungwa na Lucas Kikoti huku la wageni likifungwa na Omar Ramadhan. Ndanda walimaliza pungufu baada ya Hemed Koja kutolewa kwa kadi nyekundu.
    Ligi kuu itaendelea kesho kwa mechi mbili, Mwadui FC wakiwakaribisha Singida United mkoani Shinyanga na Lipuli FC wakiwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Samora, Iringa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR, NAMUNGO, POLISI ZAANZA VYEMA LIGI KUU, MBEYA CITY NA PRISONS 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top