• HABARI MPYA

  Wednesday, April 03, 2019

  TANZANIA PRISONS YA ADOLPH YAENDELEA KUNG’ARA, YAICHAPA MWADUI FC 2-0 SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Tanzania Prisons imeendelea kufanya vizuri chini ya kocha Mohammed Rishard ‘Adolph’ baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, Salum Kimenya dakika ya 35 na Adam Adam dakika ya 45 na kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda hadi nafasi ya saba kutoka ya tisa.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Lipuli FC imeshinda 2-0pia dhidi ya African Lyon Uwanja wa Samora mjini Iringa, mabao ya Zawadi Mauya dakika ya 60 na Miraji Athuman ‘Madenge’ dakika ya 90.
  Nayo Singida United imeichapa 2-0 Alliance FC Uwanja wa Namfua mjini Singida, mabao ya Kennedy Juma dakika ya 29 na Frank Zakaria dakika ya 45, wakati bao pekee la George Makang’a dakika ya 45 limeiapa Biashara United ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. 

  Na Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wenyeji Coastal Union wameichapa 1-0 Stand United bao pekee la Raizin Hafidh dakika ya 63.
  Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani timu ya Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya 1-1 na jirani zao, Mtibwa Sugar wenyeji wakitanguliwa kwa bao la Riphati Khamis dakika ya saba, kabla ya Fully Zully Maganya kusawazisha dakika ya 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YA ADOLPH YAENDELEA KUNG’ARA, YAICHAPA MWADUI FC 2-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top