• HABARI MPYA

    Wednesday, April 03, 2019

    SAMATTA ATOLEWA BADO DAKIKA 10 KRC GENK YACHAPWA 1-0 NA ROYAL ANTWERP UBELGIJI

    Na Mwandishi Wetu, DEURNE 
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana alitolewa dakika 10 za mwisho timu yake, KRC Genk ikichapwa 1-0 na wenyeji, Royal Antwerp katika mchezo wa hatua ya pili ya Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, maarufu kama Championship Round Uwanja wa Bosuil mjini Deurne.
    Baada ya kupambana kwa zaidi ya dakika 80 bila mafanikio, kocha Philippe Clement alimtoa Samatta dakika ya 83 na kumuingiza mshambuliaji Mbelgiji mwenzake, Zinho Gano.
    Lakini bado haikusaidia na Genk ikalala 1-0 kwa bao pekee la kiungo mkongwe wa kimataifa wa Israel, Lior Refaelov dakika ya nne.  
    Huo ulikuwa ni mchezo wa pili wa Genk katika Championship Round baada ya kushinda 3-0 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Anderlecht Machi 30, kufuatia kuongoza vizuri hatua ya kwanza ya ligi hiyo. 
    Championship Round inashirikisha timu sita ambazo pamoja na Genk, nyingine ni Club Brugge, Standard Liège, Anderlecht, Antwerp na Gent baada ya hatua ya awali, ijulikanayo kama Regular Season ambyo Genk imeongeza. 
    Na Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amecheza mechi ya 148 kwenye mashindano yote na akiwa amefunga mabao 59 tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 115 na kufunga mabao 44 na kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili na Europa League amecheza mechi 24 na kufunga mabao 14.
    Kikosi cha Royal Antwerp FC kilikuwa: Bolat, Opare, Juklerod, Refaelov/Simao dk78, Baby/Owusu dk72, Arslanagic, Lamkel Ze/Bolingi dk88, Govea, Van Damme, Haroun na Mbokani.
    KRC Genk: Vukovic, Uronen, Dewaest, Aidoo/Lucumi dk35, Maehle, Heynen, Berge, Malinovskyi, Trossard/Paintsil dk67, Ito na Samatta/Gano dk83.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ATOLEWA BADO DAKIKA 10 KRC GENK YACHAPWA 1-0 NA ROYAL ANTWERP UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top