• HABARI MPYA

  Monday, August 13, 2018

  SIMBA SC WAENDA KUMENYANA NA ARUSHA UNITED KABLA YA KWENDA KUIVAA MTIBWA MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wanatarajiwa kuondoka jioni ya leo kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Arusha United ya Ligi daraja la Kwanza.
  Simba leo wameendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gymkhana mjini Dar es Salaam, baada ya hapo wanajiandaa na safari ya kuelekea mkoani Arusha kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Jumamosi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online mjini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick J. Aussems alisema amecheza mechi mbili za kirafiki baada ya kutoka Uturuki walipoweka kambi na kuona mapungufu ya kikosi chake na kuyafanyia kazi.

  “Tunajiandaa vyema, mechi hizi ninachoangalia ni kiwango cha wachezaji wangu na kupata mwanga, kwa mechi hizi sitaangalia matokeo zaidi kwani hapo baadae nahitaji vijana wangu wafanya kile ninachowapa sasa,” alisema.
  Aussems alisema baada ya mchezo wa Arusha wataunganisha safari kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa kwa kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.
  Simba jana imerejea jijini kikitokea mkoani Lindi ambako juzi ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji, Namungo FC na kutoka sare ya bila ya kufungana katika uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa, ambao upo chini ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAENDA KUMENYANA NA ARUSHA UNITED KABLA YA KWENDA KUIVAA MTIBWA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top