• HABARI MPYA

  Tuesday, August 14, 2018

  SIMBA SC TAYARI WAPO ARUSHA, JUMATANO WANA KAZI WATOTO WA 'A TOWN'

  Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
  KIKOSI cha Simba SC kimetua Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha United Jumatano Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa mwaliko wa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
  Simba SC imefikia Masailand Safari & Lodge mjini humo na huo utakuwa mchezo wa tatu tu tangu irejee kutoka Uturuki wiki iliyopita, baada ya sare mbili 1-1 na Asante Kotoko na 0-0 na Namungo FC.
  Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Jumamosi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara.
  Wachezaji wa Simba SC wakipata chakula cha jioni katika hoteli ya Masailand Safari & Lodge mjini Arusha

  Huo utakuwa mchezo wa tatu wa kirafiki kwa timu hiyo ya kocha Mbelgiji, Patrick J. Aussems tangu kikosi kirejee kutoka Uturuki, baada ya sare mbili mfululizo, 1-1 na Asante Kotoko Dar es Salaam Jumatano na 0-0 na Namungo FC Jumamosi Ruangwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC TAYARI WAPO ARUSHA, JUMATANO WANA KAZI WATOTO WA 'A TOWN' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top