• HABARI MPYA

  Thursday, August 16, 2018

  SERENGETI BOYS YAIPIGA SUDAN 5-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA CECAFA AFCON

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ijulikanayo kama CECAFA AFCON U17 Qualifiers baada ya ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchezo wa Kundi A dhidi ya Sudan Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam leo.
  Ushindi huo unaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi sita baada ya mechi mbili na kupanda kileleni, ikiishusha Rwanda yenye pointi sita, lakini Tanzania wanapanda juu kwa wastani wao mzuri wa mabao. 

  Wachezaji wa Serengeti Boys wakishangilia ushindi wao mnono leo
   
  Omar Yousef alianza kujifunga dakika ya 10 kuipatia Tanzania bao la kwanza kabla ya Kelvin John kufunga mabao mawili dakika za 45 na 60 na Agiri Ngoda naye kufunga mawili pia dakika za 72 na 79.
  Serengeti Boys sasa wataingia kwenye mchezo mwisho na Rwanda kutafuta uongozi wa kundi kwa matarajio ya kupata mpinzani nafuu kidogo kwenye Nusu Fainali.
  Ikumbukwe Tanzania ndiyo mwenyeji wa Fainali za AFCON U17 mwakani, ambazo mfumo wake wa kufuzu sasa umebadilishwa na kuwa Kanda badala ya droo inayohusiaha bara zima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAIPIGA SUDAN 5-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA CECAFA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top