• HABARI MPYA

  Monday, August 20, 2018

  TFF YAMPA POLE MHESHIMIWA RAIS DK MAGUFULI KWA KUFIWA NA DADA YAKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa majonzi makubwa kifo cha dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt John Pombe Magufuli Bi.Monica Joseph Magufuli aliyefariki jana Agosti 19,2018 katika Hospitali ya Bugando,Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.
  Rais wa TFF ndugu Karia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho cha Bi.Monica.
  “Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli,Familia,ndugu,jamaa,marafiki na wote walioguswa na msiba huu” alisema Rais wa TFF, Karia.

  Pole Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kufiwa na dada

  Ameongeza kuwa wakati huu familia ikiwa katika majonzi makubwa TFF inaungana na wafiwa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na Mungu awape nguvu na subira.
  Mungu ametoa na Mungu ametwaa jina lake lihidimiwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAMPA POLE MHESHIMIWA RAIS DK MAGUFULI KWA KUFIWA NA DADA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top