• HABARI MPYA

    Friday, August 17, 2018

    MVUA YA MABAO YAENDELEA MICHUANO YA CECAFA KUFUZU AFCON U17

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MVUA ya mabao imeendelea katika michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ijulikanayo kama CECAFA AFCON U17 Qualifiers baada ya leo Uganda na Kenya kufanya mauaji katika mechi za Kundi B.
    Uganda ilianza kuitandika 6-1 Sudan Kusini katika mchezo uliotangulia Uweanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam kabla ya Kenya kuishindilia Djibouti mabao 9-0 katika mchezo uliofuata. 
    Mabao ya Uganda yalifungwa na Kakaire Thomas dakika za 23 na 43 na Ssekajja Davis dakika za 17, 44 na 69, wakati la Sudan Kusini limefungwa na Joseph Manase dakika ya 90.
    Wachezaji wa Kenya wakishangilia ushindi wao mnono leo dhidi ya Djibouti

    Mabao ya Kenya yamefungwa na Keith Imbali dakika za sita na 89, Said Mussa dakika ya 37, Richdonald Steward dakika za 38, 51 na 77, Nicholaus Ochieng dakika ya 60 na Mathew Malisau dakika ya 61 na 71.
    Kwa matokeo hayo, Kenya wanafikisha pointi sita baada ya mechi mbili na kupaa kileleni kwa wastani mzuri wa mabao, wakiishuhia nafasi ya pili Ethiopia yenye pointi sita pia, wakati Uganda wanaokota pointi tatu za kwanza baada ya kufungwa mechi ya kwanza.  Sudan Kusini na Djibouti zinafuatana mkiani.
    Ikumbukwe jana Tanzania ilishinda mabao 5-0 kwenye mchezo wa Kundi A dhidi ya Sudan Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam leo na kufikisha pointi sita baada ya mechi, hivyo kupanda kileleni kwa wastani mzuri wa mabao, ikiishusha Rwanda nafasi ya pili.   
    Serengeti Boys sasa wataingia kwenye mchezo mwisho na Rwanda kutafuta uongozi wa kundi kwa matarajio ya kupata mpinzani nafuu kidogo kwenye Nusu Fainali.
    Ikumbukwe Tanzania ndiyo mwenyeji wa Fainali za AFCON U17 mwakani, ambazo mfumo wake wa kufuzu sasa umebadilishwa na kuwa Kanda badala ya droo inayohusiaha bara zima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MVUA YA MABAO YAENDELEA MICHUANO YA CECAFA KUFUZU AFCON U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top