• HABARI MPYA

    Thursday, August 16, 2018

    MUX YATOA MWEZI MMOJA WAMILIKI WA VITUO VYA TELEVISHENI NCHINI KULIPIA HUDUMA, VINGINEVYO WANAFUNGIWA

    KWANZA tungependa kuishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Dk. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuongoza kwa kufuata sharia.
    Na pia tungependa kuishukuru bodi ya TCRA na Mkurugenzi wake mkuu kwa kusimamia sheria dhidi ya waendeshaji wa PAY TV ambao wamevunja sheria kuanzia mwaka 2010

    1. Kwa nini TCRA walitupatia leseni ya MUX (Multiplexer)
    Kwa nini ilikuwa lazima kuanzisha mfumo wa watoa huduma kwa ving’amuzi (MUX) katika sekta ya matangazo ya luninga?

    2. Nini lilikuwa lengo la lesseni hiyo?
    Katika kipindi baada ya mwaka 2000, vyombo vya udhibiti vilianza kupata tatizo la upungufu wa masafa (frequency), hili lilikuwa tatizo la dunia nzima, ITU na wadau wake wakakubaliana kuhamia katika masafa ya kidigitali, katika mfumo wa kianalogia unahitaji frequency moja kwa chaneli moja ya TV, wakati katika mfumoo wa kidigitali frequency moja inaweza kusafirisha kati ya chaneli 15-18 za Televisheni kupitia technologia ya DVB-T, au chaneli 20-25 kupitia teknologia ya DVB-T2 kwa kutumia teknologia ya kupunguza ya DVB-T na T2.
    Mwenyekiti wa Agape Association, Vernon Fernandes (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano wa Wamiliki wa Mitambo ya Kusambazia Matangazo ya Televisheni (MUX) leo mjini Dar es Salaam. Wengine kulia ni Mwenyekiti wa BTL, Samuel Nyalla wamiliki wa ving'amuzi vya Continental na Digitek na Justin Ndege, Mwanasheria wa Stars Times.


    3. Nani angetumia vifaa ambavyo tumesimika?
    Katika mpangilio mpya, watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kutengeneza mtandao wa kusafirishia matangazo, na vituo vya televisheni vingetengeneaza maudhui ambayo yangebebwa na watoa huduma za ving’amuzi baada ya kukubaliana malipo.

    4. Gharama za usimikaji wa mitambo?
    Watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kuweka miundombinu kama dishi, vifaa vya umeme, ama nyaya za kusafirisha matangazo kwa nje. Gharama za uwekaji wa miundombinu hutegemea ubora na chapa ya vifaa hivyo, mara nyingi inagharimu mamilioni ya dola za kimarekani kuweka miundombinu hii.
     Kwa kuongezea, watoa huduma za ving’amuzi wanahitaji kuweka miundombinu ya kurushia matangazo katika kila mikoa, gharama ya mtambo mmoja unagharimu pesa nyingi sana. 

    5. Hasara tulizopata kwa kuruhusu visimbusi vya kulipia kubeba chaneli za Bure
    Hasara zinazohusiana na namba 1: Gharama za kurusha matangazo kutoka kwa watengeneza maudhui 2: Suala la Visimbusi vya kulipia kubeba chaneli za Bure (FTA) limeathiri mauzo ya ving’amuzi na kupungua kwa malipo ya kila mwezi.

    6. Idadi waliyonayo wenye Visimbusi vya kulipia na tuliyonayo sisi vinashabihianaje?
    Ni wazi kwamba sisi kama Multiplexer, kwa pamoja tunavyo ving’amuzi vingi zaidi sokoni ukilinganisha na wale wenye huduma ya kulipia kama Azam, DSTV na ZUKU.

    7. Gharama waliyokuwa wanapata wenye vibali vya kurusha matangazo nchi nzima kabla ya kuhamia digitali, ukilinganisha na sasa baada ya kuhamia digitali.
    Kabla ya kuhamia kwenye matangazo ya kidigitali, wataoa maudhui (Chaneli za luninga) kila mmoja wao alitakiwa kujenga na kufanyia matengenezo mfumo wake wa kurushia matangazo, gharama ambazo kwa sasa zinabebwa na sisi watoa huduma za visimbuzi (Multiplexer)
    Kwa njia hii vituo vya televisheni vinapunguza matumizi makubwa katika uendeshaji wake. 

    8. Mapato yatokanayo na Matangazo ambayo wanapata huku tukiwabeba bila kulipia gharama za urushaji wa matangazo tangu mwaka 2010.
    Mapato yatokanayo na matangazo, kati ya vitu vingine yanategemea na ukubwa wa sehemu ambapo mawimbi yanafika (idadi ya ving’amuzi), kuwepo wa watoa maudhui wa chaneli za Bure katika visimbuzi vitatu (Multiplexers) kunawasaidia sehemu kubwa katika majumba ya watu hivyo, tunakuwa tuewapatia jukwaa kubwa wanalohitaji kwa ajili ya kufanya biashara ya matangazo, matangazo ya biashara hayarusiwi kwenye visimbuzi vya kulipia hivyo ilkuwa ni kosa kwa chaneli za bure kuonekana kwenye visimbuzi vya kulipia. Baada ya kuhamia digitali, kwaa sababu chaneli inaweza kurusha vipindi vingi zaidi vya ndani, hivyo ingepelekea kuongezeka kwa kiwango na ubora wa uzalishaji wa matangazo ili kuinua tasnia ya luninga, pia itakuwa maarufu na kupendwa kwenye miongoni mwa wananchi hivyoo kupata watumiaji wengi zaidi. 
    Kiujumla ukitazama mabadiliko kuingia mfumo wa kidigitali kwenye nchi mbalimbali za ITU, mapato yatokanayo na matangazo ya biashara kwa tasnia nzima ya luninga yameongezeka kwa kiwango kikubwa.

    9. Hivyo basi, kuanzia sasa –
    (1) Chaneli ambayo haitalipia ila Mtoa Huduma ya Maudhui anapaswa kuhakikisha kuwa SIGNAL yake inayoletwa kwa waendeshaji wa MUX(warushaji wa matangazo) iko katika ubora.
    Tunaweza kuweka ubora ambao tunapewa na watoaji huduma za maudhui(CSP).

    (2)Tunatoa muda wa mwezi mmoja ambaye hatolipia ada za urushaji wa matangazo atakatiwa huduma mara moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUX YATOA MWEZI MMOJA WAMILIKI WA VITUO VYA TELEVISHENI NCHINI KULIPIA HUDUMA, VINGINEVYO WANAFUNGIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top