• HABARI MPYA

  Wednesday, August 01, 2018

  AZAM FC KUMENYANA NA URA IJUMAA NAMBOOLE...WATACHEZA PIA NA KCCA, VIPERS NA ONDUPARAKA

  Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
  MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, wanatarajia kumenyana na URA Ijumaa kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo wa kwanza wa kujipima nguvu kwenye kambi yake yake Kampala, Uganda utakaofanyika Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole.
  Azam FC inaendelea na kambi yake ya wiki mbili nchini Uganda kujiandaa na msimu ujao, ambapo benchi la ufundi limekuwa likiwapa mazoezi kabambe wachezaji wa timu hiyo ili kukindaa vema kikosi hicho.
  Mbali na mechi hiyo na URA, kwa mujibu wa programu yake ikiwa nchini humo, Azam FC inatarajia kucheza mechi nyingine tatu za kirafiki dhidi ya Onduparaka, KCCA na Vipers.

  Wachezaji wa Azam FC wakiwa mazoezini mjini Kampala, Uganda leo kujiandaa na msimu mpya

  Wakati ikifikisha siku ya tatu leo jijini Kampala, Uganda, Azam FC leo Jumatano inatarajia kufanya mazoezi saa 7 mchana kwenye Uwanja wa KCCA uliopo Lugogo, jijini Kampala.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUMENYANA NA URA IJUMAA NAMBOOLE...WATACHEZA PIA NA KCCA, VIPERS NA ONDUPARAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top