• HABARI MPYA

    Thursday, February 01, 2018

    SINGIDA UNITED YAMSIMAMISHA MCHEZAJI WAKE MKONGO KWA KULETA ‘UBONDIA’ KWENYE SOKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Singida United imemsimamisha kwa muda usiojulikana mshambuliaji wake raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kambale Salita Gentil (pichani kulia) kwa utivu wa nidhamu.
    Taarifa ya Singida United kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba kwa utovu nidhamu alioufanya Kambale jana kawenye mchezo wa hatua ya 32 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) anasimamishwa mara moja.
    Kambale alimpiga ngumi mchezaji wa Green Warriors kipindi cha kwanza na kutolewa kwa kadi  nyekundu, hivyo kuiachia mzigo timu wa kucheza pungufu katika sehemu kubwa ya mchezo.
    Hata hivyo, Singida United ilishinda kwa penalti 4-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 na kusonga mbele hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAMSIMAMISHA MCHEZAJI WAKE MKONGO KWA KULETA ‘UBONDIA’ KWENYE SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top