• HABARI MPYA

  Thursday, February 01, 2018

  CHIPUKIZI PAUL PETER ASAINISHWA MIAKA MINNE AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi, Paul Peter amesaini mkataba wa miaka minne kuendelea kuichezea klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
  Mkataba huo wa kwanza kwa mchezaji huyo na klabu baada ya kupandishwa kikosi cha kwanza Azam FC, unakuja siku mbili baada ya kuisaidia timu kufuzu hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (Cup).
  Peter alifunga mabao matatu peke yake katika dakika za 52, 77 na 88 baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mbaraka Yussuf Abeid Azam FC ikishinda 5-0 dhidi ya Shupavu FC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi na kwenda hatua ya 16 Bora ya ASFC.
  Paul Peter (kushoto) akipeana mikono na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed baada ya kusaini mkataba wa miaka minne jana

  Mabao mengine ya Azam FC siku hiyo yalifungwa na chipukizi wengine, Yahya Zayed dakika ya 45 na Iddi Kipagwile dakika ya 45 na ushei.
  Tangu acheze kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza akitokea benchi na kwenda kuisawazishia timu bao ikitoa sare ya 1-1 na Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Septemba 30, mwaka jana, Peter ametokea kuwa mchezaji muhimu Azam FC.
  Kijana huyo ni za linguine la akademi ya Azam FC iliyoanzishwa mwaka 2008, ambayo inaendelea kuwa kitu muhimu katika soka ya Tanzania ikizidi kuzalisha nyota wa kabumbu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIPUKIZI PAUL PETER ASAINISHWA MIAKA MINNE AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top