• HABARI MPYA

  Friday, February 02, 2018

  REFA MBABE WA UFARANSA AFUNGIWA MIEZI MITATU

  REFA Mfaransa, Tony Chapron, ambaye alimpiga teke na akamtoa kwa kadi nyekundu mchezaji wa Nantes, amefungiwa kwa miezi mitatu.
  Chapron amepewa adhabu hiyo na Bodi ya Ligi (LFP) kufuatia tukio hilo lililotokea katika mechi Paris St Germain wanashinda 1-0 dhidi ya Nantes Januari 14.
  Aliangushwa kwa bahati mbaya na Diego Carlos wakati anakimbia, lakini akampiga teke mchezaji huyo Mbrazil kabla ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano na kumtoa kwa kadi nyekundu.
  Adhabu ya Chapron imefuatia kikao cha jana usiku cha Kamati ya Nidhamu ya LFP.

  Refa wa Ligue 1, Tony Chapron akiingia kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ya LFP jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  "Baada ya kumsikiliza Tony Chapron na kusoma taarifa ya mkufunzi, Kamati imeamua kumsimamisha kwa miezi mitatu,"imesema taarifa hiyo.
  Chapron aliomba radhi siku moja baada ya tukio hilo na kadi ya pili ya njano ya Carlos ilifutwa, ingawa Rais wa Nantes, Waldemar Kita alitaka refa huyo afungiwe miezi sita.
  Lakini inaaminika adhabu hiyo ya miezi mitatu ni kwa sababu refa huyo anastaafu mwishoni mwa msimu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA MBABE WA UFARANSA AFUNGIWA MIEZI MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top