• HABARI MPYA

  Thursday, February 15, 2018

  MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana ameendeleza moto wa mabao baada ya kuifungia timu yake, Difaa Hassan El Jadida katika sare ya 3-3 na wenyeji, Chabab Atlas Khénifra Uwanja wa Manispaa ya Khenifra kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro.
  Msuva alifunga bao lake dakika ya 42, wakati mabao mengine ya Jadida yalifungwa na watokea benchi Anouar Jayid dakika ya 82 na Adnane El Ouardy dakika ya 90 na ushei, wakati ya wenyeji yalifungwa na I. Elbas dakika ya nane, H. Merchand dakika ya 11 na K Pacero dakika ya 57.
  Simon Msuva amefunga tena jana Difaa Hassan El Jadida ikitoa sare ya 3-3 na Chabab Atlas Khénifra 
  Sare hiyo inaosogeza Difaa Hassan El Jadida nafasi ya nne kwenye msimamo wa Botola, ikifikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 16, ikiwa inazidiwa pointi sita na vinara, Raja Casablanca.
  Ikumbwe, mwishoni mwa wiki, Msuva alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 10-0 dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini.
  Kikosi kilichoanza cha Difaa Hassan El Jadida jana kilikuwa; Aziz El Qinani, Youssef Aguerdoum El Idrissi, Bakary N'diaye, Fabrice Ngah, Tarik Astati, Mohammed Ali Bemammer, Adil El Hasnaoui, Chouaib El Maftoul, Hamid Ahadad, Hamza Sanhaji na Simon Msuva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top